Shairi (GUEST POST)

Namshukuru moliwa

Kunipa hini hatua

Nikwandikie barua

Mwenye nyumba kukwetea
Ewe wangu mahashumu

Baada ya kukusalimu

Leo nimefanya hamu

Machache kukuwambia
Kuhusu yule Fulani

Maarufu ni jirani

Hakuweko asilani

Wazi nakufunulia

 

Twalikifanya mitani

Na fujo barazani

Abadani sikudhani

Matata tanietea
 Ilikuwa ni mizaha

Sikujua ni karaha

Umeshatunga usaha

Na jaraha kunitia
Nimeshashika adabu

Kidonda chanipa tabu

Na sina wakunitibu

Ila ni wewe mmoya
Mfano wa yule ngombe

Aloona ana pembe

Kinapomtoma chembe

Ni zizini huregea

 

Salamu zako ni hizi

Nataka uzimaizi

Punguza yako majonzi

Uwate kulialia
Usipandishe ghadhabu

Mahaba tukaharibu

Kusamehe ni thawabu

Pia ndio sawa ndia
Na najua wanipenda

Nami pia nina nyonda

Sitowata kukulinda

Mayamini nakulia
Na siku ni hizihizi

Hata ikawa miezi

Tutarudi kwenye enzi

Za huba na mazowea
Naeka tini kalamu

Ndio misiki khitamu

Nisongea nikushumu

Pambaja kukumbatia

By ~ Ahmed Shee Ali Alhussein

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s